1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kukiri Iran kuidungua ndege ya Ukraine kwazusha maswali

Sekione Kitojo
12 Januari 2020

Kukiri kwa Iran kuwa iliidungua ndege ya Ukraine, na kuwauwa watu wote 176 waliokuwamo, kunazusha maswali mapya juu ya uwazi katika  Jamhuri hiyo ya Kiislamu na kile kilichosababisha kuangushwa kwa ndege hiyo ya abiria.

https://p.dw.com/p/3W43Q
Hassan Ruhani
Picha: picture-alliance/dpa/Bildfunk/Iranian Presidency

Wakati  jeshi  lake  la  anga  lilikiri  na  kuchukua  jukumu, kamanda mmoja  pia  alidai  kuwa  jeshi  hilo lilionya serikali ya  Tehran kufunga  anga ya  nchi  hiyo kutokana  na  hofu  ya  Marekani kulipiza  kisasi  kutokana  na  Iran  kushambulia  kwa  makombora vituo vya  kijeshi  vilivyo  na  wanajeshi  wa  Marekani nchini Iraq.

Iran Flugzeugabsturz Ukraine International Airlines | Wrackteile bei Teheran
kikosi cha waokoaji wakitafuta vitu vitakavyotoa ushahidi kuhusu sababu za kuanguka kwa ndege ya Ukraine nchini IranPicha: Reuters/Wana/N. Tabatabaee

Kamanda  huyo  huyo  pia  amesema  alieleza  uwezekano  huo  kwa wakubwa  wake  kuwa  jeshi  lake  limeidungua  ndege  hiyo mapema  asubuhi  ya Jumatano.

Hata  hivyo , wachunguzi wa  ajali  ya  ndege  wa  Iran , maafisa  wa serikali  na  wanadiplomasia  wote walikana kwa  siku  kadhaa baadaye  kuwa  kombora  liliiangusha  ndege  hiyo chapa Boeing 737 inayoendeshwa  na  shirika  la  ndege  la  kimataifa  la  Ukraine nje  ya  uwanja  wa  ndege  wa kimataifa  wa Imam Khomenei  mjini Tehran.

"Hakukuwa  na  kombora  lililorushwa  katika  eneo  hilo katika wakati  huo," amesema  Hamid Baeidinejad , balozi  wa  Iran   nchini Uingereza, katika  mahojiano   na  kituo cha  televisheni  cha  Sky siku  ya  Ijumaa, akiyaita  maswali  mengine  juu  ya  madai  hayo kuwa  "hayakubaliki  kabisa."

Kisha  hadithi ikabadilika mapema  asubuhi  ya  Jumamosi, ambapo mkuu  wa  jeshi  la  Iran  akisema  ndege  hiyo "imelengwa bila kukusudiwa  kutokana  na  makosa  ya  kibinadamu."

Iran | Trauer und Proteste | Flugzeugabsturz
Wairan wakusanyika mbele ya chuo kikuu na kuwasha mishumaa kuwakumbuka wahanga wa ajali ya ndege ya UkrainePicha: picture-alliance/dpa/NurPhoto/M. Nikoubaz

Iran yakiri kuidungua ndege ya Ukraine

Baeidinejad  baadaye  aliomba  radhi katika ukurasa  wa  Twitter.

"Katika  taarifa yangu jana katika  chombo cha  bahari  nchini Uingereza, nilitoa matokeo rasmi ya uchunguzi yaliyotolewa na maafisa wenye  dhamana nchini mwangu kuwa  kombora halingeweza  kufyatuliwa  na  kuipiga  ndege  ya  Ukraine  katika kipindi  hicho," aliandika . " Nasikitika  kwa  kutoa  taarifa  ambazo si sahihi."

Lakini  hata  katika  kukiri kuidungua  ndege  hiyo, madai ya taarifa ya  jeshi  na  kikosi  cha  ulinzi , inazusha  maswali  ya  nani alifahamu  kuhusu  shambulio  hilo  katika  wakati  gani.

Jenerali Amir Ali Hajizadeh wa  mpango  wa  ulinzi wa  anga amesema  aliwaambia  wakubwa  wake  siku  ya  Jumatano  kuwa "tukio lililotokea  kwa  pamoja  la  kufyatuliwa  kwa  makombora  na kuanguka  kwa  ndege  kunaleta  shaka."

Wakubwa wa  Hajizadeh atakuwa  kamanda wa  juu , jenerali Hossein Salami. Kwa kawaida  kikosi  cha  ulinzi wa  anga kinawajibika  moja  kwa  moja   kwa  kiongozi  mkuu  wa  Iran Ayatollah Ali Khamenei, ambaye  ni siku  ya  Jumamosi  ndipo alipokiri  shambulio  hilo  la  kombora, akielezea  kuhusu  ripoti  ya majeshi  ya  nchi  hiyo.

Teheran Universität Studentenproteste Flugzeugabschuß Polizei
Maandamano ya wanafunzi kudai waliohusika katika kuiangusha ndege ya abiria ya Ukraine waadhibiwePicha: Getty Images/AFP/A. Kenare

Hata  hivyo  taarifa  ya  jeshji  binafsi  inazusha  maswali , wakati iliposema  ndege  hiyo ilipita "karibu  mno  na  eneo  nyeti  la  jeshi" linalomilikiwa  na  jeshi  hilo la  ulinzi  wa  anga.

Viongozi wa  kidini wanahatarisha  kutumbukia  katika  mzozo  wa uhalali wakati hasira  miongoni  mwa  wananchi  wake ikitokota kutokana  na   jinsi  taifa  hilo  lilivyoishughulikia  taarifa  ya kuanguka  kwa  ndege, ambapo  jeshi  limechukua  siku tatu  kukiri sababu  zilizosababisha  kuanguka  kwake, ikiwa  ni  kutokana  na kombora  lililofyatuliwa  kimakosa.