1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kusini kutanua ushirikiano na bara la Afrika

4 Juni 2024

Korea Kusini leo ni mwenyeji wa mkutano wa kilele na viongozi wa kiafrika ambao wamewakilishwa na wajumbe kutoka nchi 48 wakiwamo wakuu wa nchi wapatao 30.

https://p.dw.com/p/4gcpM
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk YeolPicha: JEON HEON-KYUN/Pool/REUTERS

Alipokuwa akihutubia mkutano huo mjini Seoul, Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol amesema nchi yakeitazidisha misaada ya maendeleo barani Afrika hadi karibu dola bilioni 10 ifikapo mwaka 2030 na kwamba watatanua ushirikiano wa kina hasa katika sekta muhimu za madini na teknolojia.

Soma pia:Korea Kusini yaishutumu Korea Kaskazini kwa kukiuka haki

Baada ya mkutano huo Yoon na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais wa Mauritania Mohamed Ould El-Ghazouani wanatarajiwa kutoa taarifa ya pamoja.

Hapo kesho, wakuu wa biashara wa Korea Kusini wataendesha mkutano wa kilele wa biashara utakaojikita katika masuala ya uwekezaji, maendeleo ya viwanda na usalama wa chakula.