1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Korea Kusini kusitisha makubaliano ya kijeshi na Pyongyang

3 Juni 2024

Korea Kusini inatarajia kusitisha makubaliano ya pamoja ya kijeshi na Korea Kaskazini yaliyofikiwa mwaka 2018, katikati ya ongezeko la wasiwasi wa kikanda.

https://p.dw.com/p/4gb0e
Korea Kusini| Korea Kaskazini| Mpaka
Hali kwenye mpaka wa Korea mbili imekuwa tete tangu Pyongyang iliapoanza tena kufanya shughuli zake za kijeshi.Picha: Jeonbuk Fire Headquarters/AP/picture alliance

Baraza la Usalama la Korea Kusini, NSC limesema hii leo kwamba limeamua kuyasitisha makubaliano hayo hadi kutakapofikiwa hali ya kuaminiana baina ya majirani hao, hii ikiwa ni kulingana na tangazo la ofisi ya Rais Yoon Suk Yeol. 

Pendekezo hilo linatarajiwa kupelekwa kwenye baraza la mawaziri kesho Jumanne.

Kusitishwa kwa makubaliano hayo, ambayo tayari yalivunjwa na Korea Kaskazini mwezi Novemba, kunaashiria kuanza tena kwa luteka za kijeshi karibu na mpaka unaozitenganisha Korea hizo mbili, ambazo zilisimama kufuatia  makubaliano hayo.