1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yarusha makombora ya masafa mafupi baharini

18 Machi 2024

Korea Kaskazini imerusha makombora kadhaa ya masafa mafupi yaliyoangukia baharini.

https://p.dw.com/p/4dqDq
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un azuru eneo la  mazoezi ya kijeshi
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un azuru eneo la mazoezi ya kijeshiPicha: KCNA/AFP

Korea Kaskazini imeyarusha makombora hayo wakati ambapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, yuko nchini Korea Kusini kuhudhuria mkutano wa tatu juu ya demokrasia.

Makao makuu ya jeshi la Korea Kusini yamethibitisha kurushwa kwa silaha hizo mapema Jumatatu.

Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida ameliambia bunge la nchi yake kwamba makombora yaliyorushwa na Korea Kaskazini yaliangukia baharini kwenye eneo lililopo kati ya Japan na rasi ya Korea.

Marekani imesema zoezi hilo linahatarisha usalama.