1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini na Belarus zasaini mkataba wa ushirikiano

27 Machi 2026

Viongozi wa Korea Kaskazini na Belarus wamesaini mkataba wa "urafiki na ushirikiano" siku ya Alhamisi.

https://p.dw.com/p/5BDZS
Pyongyang I Kim Jong Un na Rais Alexander Lukashenko wa Belarus
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un (kushoto) akimkaribisha kwa ukarimu Rais Alexander Lukashenko wa Belarus mjini PyongYang.Picha: Belarusian presidential press service/AFP

Mkataba huo umesainiwa baada ya Kim Jong Un kumkaribisha kwa ukarimu Rais Alexander Lukashenko  katika ziara yake ya kwanza nchini humo.

Kim na Lukashenko ambao walikutana mara ya mwisho huko China mwaka jana, wamesema katika hali ya sasa ambapo mataifa makubwa duniani yanapuuza na kukiuka waziwazi kanuni na sheria za kimataifa, ni lazima nchi huru zishirikiane kwa karibu zaidi ili kuimarisha juhudi zinazolenga kulinda uhuru na kuboresha ustawi wa raia wao.

Mbali na kuiunga mkono Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine, mataifa hayo mawili yananakabiliwa pia na vikwazo vya nchi za Magharibi na yanashutumiwa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.