Kombe la Dunia: Je, DRC itafanikiwa kufuzu?
13 Oktoba 2025
DRC ilishinda mechi dhidi ya Togo ijumaa Kwa bao 1-0 , nakurudisha matumaini Kwa DRC kufuzu kwenye kombe la Dunia baada ya kupoteza dhidi ya Senegal, mechi ambayo Kwa wakongomani ilikuwa mlango pekee wa kuingia kombe la dunia.
Kwa baadhi ya wakongomani wanaamini Kongo bado inayo nafasi ya kwenda Kwa mara ya pili kwenye kombe la Dunia.
Masudi David na Kayumba Eric ni mashabiki wa timu ya taifa, "Ushindi unamanifaa Kwa ukubwa kwasababu tulikuwa tunauhitaji ili kujihakikishia kupata nafasi ya kuweza kumpatia presha Senegal. Soka inakuwaga na maajabu yake, na lolote linaweza likatokea Senegal akatandikwa na sisi tukamtandika Sudan na tukachukuwa tiketi kibabe na tukaenda kushiriki mashindano" alisema David
"DRC kupita Moja Kwa Moja hilo tusaau kwasababu nafasi waliokuwa nayo ni dhidi ya senegali na hawakutumia nafasi hiyo vizuri na unajuwa kwenye soka Wakati mnapata fasi kama hiyo mnatakiwa kutumia vizuri kwasababu sioni timu ya Senegal kufungwa." Kayumba aliongezea.
Baada ya ushindi huo, kocha Sebastian Desabre anaamini kuwa timu yake itaenda kwenye hatua ya mchujo, "Kwetu sisi tunafikiria kuwa tukishinda mechi tatu zinazo tutaenda kwenye mchujo wa kombe la Dunia"
DRC inajiandaa kukipiga dhidi ya Sudani kesho Wakati wakiombea Senegal ifungwe au Kongo ichukuwe nafasi ya timu 4 zitakazo pambana kutafuta timu itakayoenda kwenye mchujo .
Ramazani Kahambwe mchambuzi wa michezo anatoa maoni yake kuhusu timu ya Kongo, "Matumaini yetu ni makubwa sana kufuzu kama mshindi Bora wa nafasi ya pili, Kongo asilimia kubwa huwa tunapita tukiwa na kikokotoo mkononi, lakini ile ya kusema kwamba hii mechi tunauhakika nayo Kwa asilimia mia mara nyingi huwa atufuzu."
"Siyo kazi rahisi lakini ukiingia vitani lazima ujipange kwaajili ya mapambano. Hayo Mataifa mengine nao pia wanajuwa kwamba Afrika Kuna Watu watatoka huko ni wahatari sana. Hata hivyo, DRC bado safari ni ndefu kwani timu 4 zitachuana ili kutafuta timu Moja itakayo wakilisha Afrika kwenye mchujo utakao shirikisha mabara tofauti"
Bara la Afrika litawakilishwa na timu tisa zitakazo fuzu moja kwa moja, tano miongoni mwao tayari zimejikatia tiketi zao, nazo ni Tunisia, Moroko, Algeria, Misri na Ghana.
Mnamo mwaka wa 1934, Misri ilikuwa timu ya kwanza ya Afrika kushiriki katika fainali za Kombe la Dunia. Wakati DRC, ikijulikana kama Zaire Ilishiriki katika michuano hiyo mnamo mwaka 1974, na kuwa timu ya kwanza ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kufuzu.
Senegal inaongoza Kundi B, na alama 21. huku DRC ikichukuwa nafasi ya pili na alama 19.