1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa zamani wa waasi Kongo ahukumiwa miaka 30 jela

16 Desemba 2025

Aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Roger Lumbala amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa ya ukatili aliofanya miongo miwili iliyopita wakati wa Vita vya Pili vya Kongo.

https://p.dw.com/p/55Tgr
Roger Lumbala
Kiongozi wa waasi wa M23 nchini Kongo, Roger LumbalaPicha: Isaac Kasamani/AFP/Getty Images

Lumbala alipatikana na hatia katika mahakama ya jinai ya Paris kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Wakili wa Lumbala, ambaye ana siku kumi za kukata rufaa, ameitaja hukumu hiyo kuwa kali.

Lumbala mwenye umri wa miaka 67 aliongoza kundi la waasi wa Kongo kwa ajili ya Demokrasia ya Kitaifa, lililodaiwa kuungwa mkono na Uganda na kushtumiwa kwa ukatili dhidi ya raia, hasa kwa kuzilenga jamii za makabila madogo ya Nande na Bambuti mashariki mwa Kongo kati ya mwaka 2002 na 2003.

Waathiriwa wa dhulma hizo wamepongeza hukumu hiyo na kusema hatimaye haki imepatikana.