1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Kiongozi wa upinzani India awataka raia kupinga 'udikteta'

11 Mei 2024

Mpinzani wa Narendra Modi, Arvind Kejriwal, amewataka wafuasi wake kupinga kile alichokiita kuwa "udikteta", baada ya mahakama kuu ya nchi hiyo kumwachilia kwa muda kutoka jela kufanya kampeni za uchaguzi

https://p.dw.com/p/4fjv5
Waziri kiongozi wa jimbo la Delhi Arvind Kejriwal akiwahutubia wafuasi wake mjini New Delhi mnamo Februari 25,2024
Waziri kiongozi wa jimbo la Delhi Arvind KejriwalPicha: Hindustan Times/IMAGO

Katika mkutano na waandishi wa habari siku moja baada ya kuachiliwa kwake, Kejriwal, ambaye ni waziri kiongozi wa jimbo la Delhi linalojumuisha mji mkuu wa India amesema, kuwa matokeo yauchaguzi huo yataamua iwapo taifa hilo litasalia kuwa taifa la demokrasia.

Kejriwal ameongeza kuwa amekuja kuomba watu bilioni 1.4 kuiokoa nchi yake.

Modi ashtumiwa kwa kuwalenga

Kiongozi huyo wa upinzani alimshutumu Modi kwa kuwalenga wapinzani wake kwa kutumia uchunguzi wa uhalifu dhidi yao na kuongeza kuwa waziri huyo mkuu ameanza harakati hatari sana na kwamba atawapeleka viongozi wote wa upinzani jela.

Kejriwal, kiongozi mkuu wa upinzani katika muungano ulioundwa kumpinga Modi katika uchaguzi huo, aliachiliwa kwa dhamana jana Ijumaa baada ya kuwa rumande kwa wiki kadhaa .