1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

India kuanza duru ya pili ya uchaguzi

26 Aprili 2024

Uchaguzi nchini India unarejea tena hii leo, huku mamilioni ya watu wakitarajiwa kupiga kura katika baadhi ya maeneo yanayokabiliwa na joto kali.

https://p.dw.com/p/4fCSu
India | Waziri Mkuu Narendra Modi
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi anatarajiwa kushinda kwenye uchaguzi unaoendelea kwa awamu ya pili nchini humoPicha: ANI Photo/Hindustan Times/Sipa USA/picture alliance

Waziri Mkuu Narendra Modi anatarajiwa kushinda kwa awamu ya tatu katika uchaguzi huo mkubwa kabisa ulimwenguni unaokamilika mapema mwezi Juni.

Hata hivyo, idadi ya wapiga kura waliojitokeza katika duru ya kwanza ilishuka kwa karibu asilimia 66 ikilinganishwa na mwaka 2019, na baadhi ya vyombo vya habari vya India vilisema joto kali liliwazuia wengi kujitokeza.

Duru hii ya pili inayofanyika kwa awamu ili kupunguza mzigo wa uendeshaji itahusisha majimbo 13 na maeneo yanayokabiliwa na joto la zaidi ya digrii 40 za Celsius, ambayo ni pamoja na Bihar, lenye idadi kubwa zaidi ya watu na kitovu cha madhehebu ya Hindu.