1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKorea Kaskazini

Kim ahimiza "mabadiliko muhimu" katika maandalizi ya vita

15 Mei 2024

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amehimiza kufanyike kile alichokiita "mabadiliko muhimu" katika maandalizi ya vita kwa kulenga vituo vya kutengeneza silaha.

https://p.dw.com/p/4frH1
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong UnPicha: YONHAPNEWS AGENCY/picture alliance

Wakati akikagua mfumo wa ulinzi wa anga wa nchi yake, Kim ameonyesha kuridishwa na kasi ya viwanda vya Korea Kaskazini ya kutengeneza silaha mwaka huu.

Kauli ya kiongozi huyo inatokea wakati wachambuzi wakieleza kuwa Korea Kaskazini inanuia kufanya majaribio ya silaha na kuongeza utengenezaji wa makombora ili kuipa Urusi kwa ajili ya matumizi katika vita vyake dhidi ya Ukraine.

Soma pia:  Kim Jong Un asimamia na kukagua urushaji wa kombora jipya

Nchi hiyo iliyotengwa kimataifa, hivi karibuni imeimarisha uhusiano wa kijeshi na Urusi huku Korea Kaskazini ikiishukuru Moscow kwa kutumia kura yake ya turufu kuzuia kuanzishwa upya kwa jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaofuatilia vikwazo vya kimataifa vya silaha dhidi ya utawala wa Kim.

Korea Kusini na Marekani zimeishutumu Korea Kaskazini kwa kuipa Urusi silaha licha ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa kupiga marufuku hatua hiyo.