1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiapo cha rais Putin kuongoza Urusi

Sudi Mnette
8 Mei 2018

Tahariri ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani imejikita katika kuapishwa Kiongozi wa Urusi Vladimir Putin  hapo jana (07.05.2018) na kumfanya sasa awe rais kwa muhula wa nne.

https://p.dw.com/p/2xM3g
Russland Altbundeskanzler Schröder bei Putins Amtseinführung
Rais Vladimir Putin akisalimiana na Kansela wa zamani wa Ujerumani Gerhard SchröderPicha: picture-alliance/AP/SPUTNIK KREMLIN/A. Druzhinin

Katika uhariri wake Kolner Stadt-Anzeiger linalotoka mjini Cologne limeandika juu ya  kile anachojivunia Putin wakati akiingia  muhula wa nne wa utawala wake. Linaandika kuwa Putin anasherehekea miujiza mipya ya silaha na mashujaa wake wa vita. Lakini ilionekana kama kwamba  anajivunia pia  maajabu ya kiuchumi  ambayo katika hali halisi hayapo. Pato  limebakia kama lilivyo kwa miaka mingi sasa, wenye maarifa wanakimbilia nchi za nje, ukandamizaji wa wapinzani wake limekuwa takriban jambo la kila siku. Pamoja na yote hayo, Putin anazidi kung'ara, akitoa sura ya  kwamba Urusi inakwenda sambamba na yale yaliokuweko enzi za muungano wa Kisovieti."

Russland Altbundeskanzler Schröder bei Putins Amtseinführung
Rais Vladimir Putin akisalimiana na Kansela wa zamani wa Ujerumani Gerhard SchröderPicha: picture-alliance/AP/SPUTNIK KREMLIN/A. Druzhinin

Gazeti la  Badische Zeitung linalotoka mjini Freiburg, nalo limejikita katika mada hiyo ya muhula wa nne wa rais Putin na haja ya kujenga hali ya kuaminiana kati ya Urusi na nchi za magharibi. Gazeti hilo linaandika kuwa Kile kilichowazi ni kwamba Urusi na upande wa  magharibi zimeingia katika  hatua ya Putin na muhula wake wa nne. Putin anaendelea kuwa Rais na kutokana na hayo yeye na wenzake wa magharibi, watakuwa na kazi ya kujenga  hali ya kuaminiana, jambo ambalo Rais wa  zamani wa Marekani Barack Obama alilipigania  lakini kikweli hakujaribu kulifikia  na ambalo ni muhimu katika kuleta wizani na kupigania kwa dhati hali ya kuaminiana kati ya Mashariki na Magharibi.

Frankfurter Allgemeine Zeitung,  linaandika kuwa , hotuba ya Putin hapo jana Jumatatu baada ya kuapishwa ,ilielekea upande tafauti kabisa. Linasema Vladimir Putin aligusia  maswala kadhaa. Lakini kukithiri kwa rushwa ni utaratibu wa utawala wake, kutofanya kazi barabara kwa sheria panapohusika na  wajasiriamali wadogo na  wa tabaka la kati ni matukio ya kila siku yakiandamwa na urasimu mkubwa.

Kuhakikisha ushindi wake, kulitegemea sera zake za ndani, jambo ambalo pia lilizingatia  uhusiano wa Putin na ulimwengu  uliosalia. Anapozungumzia amani,  majadiliano na  ushirikiano  katika hali ya usawa, kuna watakaopongeza ,kwa kusema  kuwa Urusi  kuna demokrasia, wakati sivyo hata kidogo Na hapo ndipo inaposhangaza  kumuona Kansela wa zamani wa Ujerumani Gerhard Schröder akiwa mstari wa mbele kwenye sherehe ya kuapishwa mtawala huyu, Vladimir Putin.

Gazeti la Die Welt linalotoka mjini Berlin , lilijikita pia na kuwepo kwa  Kansela wa zamani wa Ujerumani Schöder katika hafla ya jana ya kuapishwa rafiki yake Putin. Katika hali ya kutofurahishwa na kuhudhuria kwake, gazeti hilo limeandika kwamba Inasumbua mno kumuona  Kansela wa zamani wa Ujerumani akiwa katika hafla hiyo. Na muhimu nyuma ya Schröder alikuwa ni mcheza sinema Steven Seagal ambaye mafanikio yake ya mwisho yalikuwa ni miaka 20 iliopita. Kila unapoendelea kuiangalia picha ile ya kufedhehesha ndipo inapokuwa wazi kwamba hapa ndipo Schöder alipofikia. Ni Steven Seagal wa siasa za kimataifa.

Mwandishi : Mohammed Abdul-Rahman/Inlandspresse
Mhariri:Yusuf Saumu