Kesi dhidi ya Oscar Pistorius yaahirishwa | Michezo | DW | 28.03.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Kesi dhidi ya Oscar Pistorius yaahirishwa

Kesi ya mauwaji inayomkabili mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius imeahirishwa hadi Aprili 7, kwa sababu mmoja wa wataalamu wa sheria ambaye atamsaidia jaji kufikia uamuzi, ni mgonjwa

Hali hiyo ilimaliza matarijio ya jana Ijumaa kuwa mwanariadha huyo mwenye ulemavu wa miguu aneingia kizimbani kutoa ushahidi kuhusiana na tukio ambalo alimpiga risasi na kumuua mchumba wake Reeva Steenkamp.

Jaji Thokozile Masipa alitangaza mahakamani kuahirishwa kesi hiyo katika siku ambayo mawakili wa Pistorius walitarajiwa kuanza kuwasilisha hoja zao baada ya wiki nne za kutoa ushahidi kutoka upande wa mashitaka.

Pistorius anakabiliwa na adhabu ya kifungo cha miaka 25 gerezani kama atapatikana na hatia ya kumuuwa makusudi Steenkamp, na pia huenda akatupwa jela kwa miaka mingi kama atahukumiwa kwa mauaji ya bila kukusudia au mauwaji ya kughafilika.

Mwanariadha huyo anasema alimpiga risasi Steenkamp kwa ajali, baada ya kumdhania kuwa jambazi aliyevamia nyumbani kwake, na hapo ndipo alipofyatua risasi kupitia mlango uliofungwa wa choo katika saa za alfajiri za Februari 14 mwaka wa 2013. Waendesha mashitaka wanasema alimuua Steenkamp baada ya mabishano. Pistorius amekanusha mashitaka ya mauwaji na pia kukana mashitaka mengine matatu yanayohusiana na umiliki wa silaha.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu