Katiba mpya nchini Kenya yajadiliwa
17 Novemba 2009Jana mswada wa katiba hiyo ulichapishwa, na wananchi sasa wamepewa mwezi mmoja kuujadili na kutoa maoni yao kwa kamati ya mabingwa ambao walioitunga hati hiyo.Mwenyekiti wa kamati iliotunga mswada huo, Nzamba Kitonga, alisema huo ni mswada wa kuweza kuweko mdahalo miongoni mwa Wakenya. Miongoni mwa mapendekezo ya mswada huo ni kuwa na waziri mkuu mwenye madaraka ya utendaji, mabaraza mawili ya bunge, madaraka yasambazwe mikoani na vijijini, kubakishwe mahakama za Kiislamu za kadhi, na kwamba mawaziri wa serikali wasizidi 20, nusu yao wakitokea nje ya bunge.
Baada kuchapishwa mswaada huo, Othman Miraji alifanya mahojiano ya simu na waziri wa Kenya wa sheria na masuala ya katiba, Mutula Kilonzo: vipi anavoutathmini mswada huo.
Mtayarishaji: Othman Miraji
Mpitiaji: Mohamed Abdulrahman