1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabendera aachiwa huru

24 Februari 2020

Mwandishi wa habari za uchunguzi nchini Tanzania, Eric Kabendera leo ameachiwa huru na mahakama ya kisutu baada ya kukiri makosa yake.

https://p.dw.com/p/3YKB0
Tansania Gericht in Kisutu | Prozess Journalist Erick Kabendera
Picha: DW/S. Khamis

Mwandishi wa habari za uchunguzi nchini Tanzania, Eric Kabendera leo ameachiwa huru na mahakama ya kisutu baada ya kukiri makosa yake na mahakama hiyo kumwamuru kulipa fidia ya zaidi ya shilingi milioni 200 kwa makosa yote aliyokuwa akituhumiwa. 

Mwandishi huyo aliyesota jela kwa zaidi ya miazi sita, sasa amerejea uraini na hatua ya kuachiliwa kwake inafuatia makubaliano aliyoyafikia Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Kupitia makubaliano hayo, Kabendera aliyekuwa akishtakiwa kwa makosa matatu,amekiri mashtaka mawili ya kukwepa kodi ya zaidi ya shilingi milioni 173 na utakatishaji wa fedha kiwango kama hicho hicho. Kama sehemu ya makubaliano hayo, Kabendera aliyefiwa na mama yake mzazi hivi karibuni wakati akiwa gerezani amekubali kulipa kiasi cha shilingi milioni 172 kwa kipindi cha miezi sita kuanzia sasa.

Journalist Erick Kabendera Tansania
Mwandishi Kabendera wakati alipokuwa akitoka kwenye moja ya mashauri yake.Picha: DW/S. Khamis

Kadhalika amelipa kiasi cha shilingi 250,000 za Tanzania kama faini na iwapo angeshindwa kulipa kiasi hicho cha fedha angetumikia kifungo cha miezi sita jela. Na Katika kosa la pili la kutakatisha fedha Kabendera tayari amelipa faini ya shilingi milioni 100.

Baada ya kutimiza masharti hayo, Kabendera ambaye amekuwa akiviandikia vyombo vya magharibi aliachiwa kutoka mikononi mwa askari magereza na baadaye alipokutana na waandishi wa habari alikuwa na haya ya kusema.

Kuachiliwa kwake kunafuatia ombi aliloliwasilisha hivi karibini kwa mkurugenzi wa makosa la kutaka kuachiliwa huru.

Katika meizi ya hivi karibuni mkurugenzi huyo aliwaachiwa watuhumiwa kadhaa waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi baada ya kukiri makosa yao na kuamuliwa kurejesha fedha zilizokubaliwa.

Mwandishi huyo wa habari alikamatwa Julai 2019 akiwa nyumbani wake akituhumiwa kukwepa kulipa kodi, kutakatisha fedha na kuongoza genge la uhalifu. Awali maafisa wa polisi walisema kuwa kukamatwa kwake kulitokana na kutiliwa shaka uraia wake, lakini baadaye ripoti za jeshi hilo zilisema alikuwa akishikiliwa kwa makosa hayo matatu.

Kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu pamoja na taasisi zizoangazia maslahi ya wanahabari zilizotaka kuchiwa kwa mwandishi huyo.