J2 16.06 EU Luxemburg | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 16.06.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

J2 16.06 EU Luxemburg

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Steinmeier ambaye ametoa ushauri wa kuiacha Ireland kando katika mchakato wa kuleta ujumuisho katika umoja wa Ulaya kutokana na nchi hiyo kuukataa mkataba wa Lisbon.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Steinmeier ambaye ametoa ushauri wa kuiacha Ireland kando katika mchakato wa kuleta ujumuisho katika umoja wa Ulaya kutokana na nchi hiyo kuukataa mkataba wa Lisbon.Tatizo linalohusu mkataba wa Lisbon linapaswa kwanza kushughulikiwa, na wahusika katika umoja wa Ulaya. Hali itakuwaje ili kusonga mbele. Leo hii mawaziri wa mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya watalizungumzia suala hilo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier tayari ameliweka suala la kura ya maoni iliyofanyika hivi karibuni nchini Ireland kuwa moja kati ya mada katika mkutano wa umoja huo.Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier anadiriki kuwa mtu wa kwanza kutoa pendekezo ambalo si rahisi , kwamba umoja wa Ulaya unaweza kufanyakazi bila ya Ireland. Kura ya hapana iliyopigwa na wapigakuwa wa Ireland , kwa mara nyingine tena kundi hilo la mataifa wanachama 27 limeingia katika mzozo mwingine mkubwa, na mawaziri wa mambo ya kigeni , wameingia katika kazi ya kutafuta njia ya kujitoa. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeire amesema kuwa,

pamoja na hayo , inawezekana, kuwa Ireland ilikuwa inajitafutia njia kwa muda mrefu kujitoa katika umoja wa Ulaya, pamoja na kujitoa katika uboreshaji wa hatua za ujumuisho , na sasa wanapaswa kukaa kando ili tuweze kuuimarisha mkataba wa Lisbon kwa kupitia mataifa 26 yaliyobaki.

Waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Ujerumani anataka mpango wake huo upatiwe muda wa kuangaliwa na wenzake katika mkutano wao mjini Luxemburg, na iwapo yeye pamoja na wenzake wanaweza kulipima hilo, inawezekana kuwa ni suala lenye shaka shaka. Ufaransa, Poland na Uingereza tayari wametoa ishara, ya kuwa na hofu kuwa mataifa mengine yanaweza kuutupa mkataba huo kando kwa kura ya hapana pia.

Kura ya pili ya hapana inaweza kuuingiza mkataba huo wa Lisbon katika matatizo zaidi, na kuukwamisha kabisa, na hali hiyo serikali ya Uingereza inataka iepukwe, kutokana na kwamba toka hapo Uingereza ilikwisha toa vipengee kadha vya kujifaidia katika mkataba huo.


Kuidhinishwa kwa mkataba huo wa mageuzi katika kila nchi kutaendelea, hilo ni moja. Kura ya hapana ya Ireland ni kama chombo kilicholeta somo na kujitambua, kwa umoja huo. Ndio sababu leo mchana inawezekana pia ujumbe wote wa Ireland kuwajibika zaidi. Ni kitu gani mataifa ya Ulaya yameweza kupata mwanga wa matumaini, ni suala ambalo liko mikononi mwa viongozi wa mataifa ya Ulaya waliokutana mjini Luxemburg kama anavyosema kiongozi wa Luxemburg Jean-Claude Juncker.

Tunapaswa kujiingiza katika mazungumzo ya maana kutokana na kura hiyo ya hapana ya Ireland kutuhusu sisi. Na baadaye tutaona , vipi tunaweza kujitoa katika hali hii ambayo si nzuri.

Tunaamini kuwa tunaweza kuendelea na utaratibu wetu na kuchukua pendekezo la Ireland ama majadiliano mengine hapo baadaye.

Kama walivyo mawaziri wa mambo ya kigeni , baadaye wiki hii viongozi wa serikali watakuwa na majadiliano kuhusiana na kura hiyo ya hapana iliyopigwa na wapigakura wa Ireland na mada ni kuwa watafanya nini kusonga mbele, swali hilo litasubiri hadi , hadi pale mataifa hayo ya umoja wa Ulaya yatakapoweza kujitoa katika mzozo huo mpya.

►◄
 • Tarehe 16.06.2008
 • Mwandishi Kitojo, Sekione
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EKSS
 • Tarehe 16.06.2008
 • Mwandishi Kitojo, Sekione
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EKSS
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com