ISRAEL | Matukio ya Kisiasa | DW | 04.02.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

ISRAEL

Nchini Israel kumetokea shambulio la kujitoa mhanga, katika eneo lenye maduka ambapo mwanamke mmoja ameuawa na watatu wengine 11 kujeruhiwa.

default

Askarai wa Israel wakiuchunguza mwili wa mpalestina aliyejilipua huko Danoma kusini mwa Israel leo.

Makundi matatu ya kijeshi ya kipalestina likiwemo kundi la  Popular Front for the Liberation of Palestina PFLP  yamedai kuhusika na shambilio hilo.


Kundi hilo la PFLP ni tawi la kijeshi la chama cha Fatah cha Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahamoud Abbas.


Kundi linalojiita mashujaa wa brigedi ya Al Aqsa ambalo ambalo kwa sasa limeacha kunasibishwa na chama cha Fatah cha Rais Mahamoud Abbas limedai kushirikiana kufanya shambulizi hilo na jeshi hilo la PLFP pamoja na kundi lingine liitwalo Unified Resistance Brigade.


Afisa wa ngazi ya juu wa kundi hilo la Al Aqsa, Abu al- walid amesema kuwa washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga wanatoka Gaza na kwamba maandalizi la shambulizi hilo huko kusini mwa Israel waliyafanyia Ramallah mji mkuu wa Ukingo wa Magharibi.


Lakini chama cha Fatah kimekanusha kuhusika na shambulizi hilo katika mji wa Dinoma ambako kuna mtambo wa nuklia.


Katika shambulizi hilo mtu mmoja alijilipua katika eneo la maduka la Dimona, ambapo mshambuliaji wa pili alishindwa kujilipua baada ya kujeruhiwa na mlipuko wa kwanza.


Hiyo iligundulika pale alipokuwa miongoni mwa majeruhi waliyofikishwa hospitali kwa ajili ya matibabu, ambapo alibainika kuwa na bomu kiunoni.


Dr Baruch Mandeltzwieg aliyekuwa akiwatibu majeruhi hao alisema kuwa alibaini mkanda wenye mlipuko kiunoni mwa majeruhi huyo wakati alipokuwa akitaka kumfayia upasuaji.


Amesema kuwa mtu huyo alijaribu kunyoosha mikono kutaka kujilipua lakini polisi waliyokuwa karibu waliwahi kumpiga risasi na kumuua.


Mara baada ya shambulizi hilo Israel ilifanya mashambulizi huko Gaza ambapo watu wawili waliuawa akiwemo afisa wa juu wa wanamgambo wa kipalestina.


Lakini msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje ya Israel Arje Mekel amesema kuwa hakuna uhusianao wowote wa shambulizi hilo na kushambuliwa kwa maduka kusini mwa nchi hiyo.


Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahamoud Abbas mbali ya kulaani shambulizi la Dimona pia alilaani mashambulizi ya Israel huko Gaza.


Hatua ya shambulizi hilo la huko Dinoma linaonekana kuzikwaza juhudi za kufufuliwa kwa mazungumzo ya amani baada ya miaka saba ya kutokuwepo kwa mazungumzo hayo.


Toka harakati hizo zianze mapema mwezi Novemba mwaka jana kiasi cha watu 150 wamekwishauawa wengi wakiwa ni wapalestina wa Gaza katika mashambulizi tofauti.


Israel imekuwa ikiwalaumu wanamgambo wa Hamas kufanya mashambulizi ya maroketi kutokea Gaza, hali iliyoifanya kuufunga mpaka wake na eneo hilo na kupelekea dhiki kubwa ya mahitaji ya kibinaadamu ikiwemo nishati ya petroli.

 • Tarehe 04.02.2008
 • Mwandishi Liongo, Aboubakary Jumaa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/D2CS
 • Tarehe 04.02.2008
 • Mwandishi Liongo, Aboubakary Jumaa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/D2CS

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com