1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yawaua wanamgambo wanne katika eneo la Rafah

9 Februari 2026

Jeshi la Israel limewaua washukiwa wanne wanamgambo waliokuwa wamejihami na silaha walipojitokeza kutoka kwenye handaki katika eneo la Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/58M7E
Jeshi la Israel limewaua watu wanne wanaoshukiwa kuwa wanamgambo baada ya kujitokeza kutoka kwenye handaki huko Rafah.
Jeshi la Israel limewaua watu wanne wanaoshukiwa kuwa wanamgambo baada ya kujitokeza kutoka kwenye handaki huko Rafah.Picha: Israeli Army/REUTERS

Jeshi la Israel limesema limewaua watu wanne wanaoshukiwa kuwa wanamgambo waliowashambulia vikosi vake wakati wanaume hao waliokuwa na silaha walipotoka kwenye handaki katika eneo la Rafah kusini mwa Gaza.

Jeshi limethibitisha katika taarifa yake kwamba magaidi wanne wenye silaha walitoka kwenye handaki la chini ya ardhi na kuwafyatulia risasi wanajeshi eneo la Rafah na baada ya kutambuliwa, wanajeshi wakawaangamiza magaidi hao.

Jeshi pia limesema hakuna mwanajeshi aliyejeruhiwa katika shambulizi hilo dhidi ya maafisa wake ambalo limelieleza kuwa ni ukiukaji wa makubaliano ya usitishaji mapigano katika Ukanda wa Gaza kati ya Israel na Hamas.