1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Saumu Mwasimba
5 Desemba 2023

Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti leo, kwamba jeshi la nchi hiyo limeyashambulia maeneo yaliyoko karibu na mji wa Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4ZnJx
Nahostkonflikt | Ende der Waffenruhe | Luftangriff auf Khan Yunis
Mji wa Khan Younis kusini mwa Ukanda wa GazaPicha: Mahmud Hams/AFP/Getty Images

Gazeti la Times nchini humo limenukuu ripoti za Wapalestina, likisema wanajeshi wa Israel wameanza mashambulizi makali ya mabomu kuelekea maeneo ambayo wameyafungamanisha na kundi la Hamas, katika mji huo. Mashirika ya misaada yameelezea juu ya kuwepo mateso makubwa yasiyokubalika yanayowakabili raia. Kwa mujibu wa jeshi la Israel, mapema leo asubuhi  milio ya ving'ora vya tahadhari juu ya kutokea mashambulio ya anga, ilisikika katikamiji chungunzima  ikiwa ni pamoja na mji wa Kibbutz karibu na mpaka baina ya Israel na Gaza. Kwa hivi sasa vikosi vya mapambano ya ardhini vya Israel vinaendelea na mashambulizi vikilisogelea eneo hilo la Kusini mwa Ukanda wa Gaza.