1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel: Hatujawashawambulia wapalestina Kaskazini mwa Gaza

Sylvia Mwehozi
15 Machi 2024

Wizara ya afya ya Palestina imevituhumu vikosi vya Israel kwa kufanya shambulizi karibu na kituo cha usambazaji wa misaada, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza na kuwaua watu 20 na kuwajeruhi wengine 155.

https://p.dw.com/p/4dak1
Mzozo wa Mashariki ya Kati |Khan Yunis
Maafa ya mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza Picha: Yasser Qudih/Xinhua/IMAGO

Jeshi la Israel limekanusha ripoti hizo, ilizozitaja kuwa za uongo na kuongeza kwamba itachunguza kwa kina kuhusu vurugu hizo zilizotokea jana jioni. 

Jumuiya ya kimataifa imekuwa ikishinikiza misaada zaidi kupelekwa Gaza, katikati mwa ongezeko la mgogoro wa kibinadamu na vizuizi vya Israel vinavyotatiza misaada kuingia kwa njia ya barabara. 

Bado hakuna mwelekeo wa amani kati ya Israel na Hamas

Meli iliyobeba tani 200 za vyakula imewasili kwenye pwani ya Gaza mchana huu ikitokea Cyprus.

Wakati huohuo, Australia imetangaza mapema leo kwamba itarejesha ufadhili kwa shirika la Umoja wa Mataifa linalotoa misaada kwa Wapalestina la UNRWA, na kuahidi nyongeza ya fedha kwa shirika la UNICEF ili kutoa huduma za haraka huko Gaza.