1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yafungua tena mpaka wa Rafah ‘kwa majaribio’

1 Februari 2026

Mpaka wa Rafah, unaounganisha Misri na Ukanda wa Gaza, umefunguliwa tena leo baada ya kufungwa kwa takriban mwaka mmoja, ingawa masharti makali bado yanatumika.

https://p.dw.com/p/57pFy
Palestina-Rafah
Vyanzo vya Kipalestina vimesema wagonjwa ndio watakaoanza kuruhusiwa kutoka Gaza.Picha: Bashar Taleb/AFP/Getty Images

Kwa sasa, ufunguzi huo unafanyika kwa majaribio, na watu hawataruhusiwa kuvuka mpaka hadi kesho, kutokana na majadiliano yanayoendelea kuhusu usalama na taratibu za uendeshaji.

Msemaji wa Israel amethibitisha hatua hiyo, huku vyanzo vya Kipalestina vikisema kuwa wagonjwa takriban 50 ndio watakaoanza kuruhusiwa kutoka Gaza pamoja na walezi wao.

Hata hivyo, vyanzo vya usalama vya Misri vinasema upande wa Palestina bado haujafunguliwa, kwani jeshi la Israel linaendelea kuudhibiti mpaka tangu kusitishwa kwa mapigano mwezi Oktoba.

Ufunguzi wa mpaka huu ni sehemu ya mpango wa amani wa Rais wa Marekani Donald Trump, na unajiri baada ya kundi la  Hamas kukabidhi mabaki ya mateka wa mwisho wa Israel waliokuwa wanashikiliwa Gaza.