1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yadai kupata miili mitatu ya mateka Gaza

24 Mei 2024

Jeshi la Israel limedai kuwa miili mitatu ya mateka waliokamatwa na wanamgambo wa Kipalestina wakati wa uvamizi wa Oktoba 7 imepatikana leo katika eneo yanakoendelea mapigano kwenye Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4gFrq
Mwanajeshi wa Israel kwenye mji wa kusini mwa Ukanda wa Gaza, Rafah.
Mwanajeshi wa Israel kwenye mji wa kusini mwa Ukanda wa Gaza, Rafah.Picha: IDF/Xinhua/picture alliance

Wiki iliyopita, jeshi la Israel lilisema kuwa miili mingine minne ya mateka ilipatikana kwenye mahandaki katika eneo la Jabalia.

Soma zaidi: Israel yafanya mashambulizi mabaya katika ukanda wa Gaza

Israel ilitangaza vita dhidi ya wanamgambo wa Hamas na makundi mengine ya Kipalestina, baada ya wanamgambo hao kuvamia eneo la kusini mwa Israel, ambako watu 1,200 waliuawa na wengine wengine 250 kushikiliwa mateka.

Soma zaidi: ICJ yaiamuru Israel kusitisha mashambulizi Rafah

Tangu hapo, mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 35,000, wengi wao wanawake na watoto, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas.