ISLAMABAD:Polisi watumia gesi kukabiliana na waandamanaji | Habari za Ulimwengu | DW | 30.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD:Polisi watumia gesi kukabiliana na waandamanaji

Polisi nchini Pakistan wamelazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi na risasi za mpira dhidi ya mamia ya waandamanaji wakiwemo wanasheria wanaopinga hukumu ya mahakama kuu iliyomruhusu Rais Pervez Musharraf kugombea tena urais.

Hukumu hiyo inafuatia kesi iliyofunguliwa na upande wa upinzani uliyokuwa ukipinga Generali Musharraf kuwania kiti hicho wakati akiwa bado na cheo cha ukuu wa majeshi.

Tayari tume ya Uchaguzi nchini humo imekwishamuidhinisha General Musharraf kuwania tena kiti hicho cha urais katika uchaguzi mkuu wa wiki ijayo.

Hata hivyo upande wa upinzani umesema kuwa unajiandaa kwa juhudi nyingine za kisheria dhidi ya kiongozi huyo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com