1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yasema mwandamanaji Erfan Soltani hajahukumiwa kifo

15 Januari 2026

Mwandamanaji mmoja wa Iran Erfan Soltani, mwenye umri wa miaka 26, ambaye Marekani ilihofia atanyongwa, hatahukumiwa kifo. Haya yamesemwa leo na idara ya mahahakama ya Iran.

https://p.dw.com/p/56qp2
Iran |  Erfan Soltani
Mwandamanaji wa Iran Erfan Soltani, mwenye umri wa miaka 26, ambaye Marekani ilihofia atanyongwa.Picha: Hengaw Organisation for Human Rights/X

Mahakama hiyo imesema Soltani hajahukumiwa kifo na ikiwa atapatikana na hatia, kulingana na sheria, adhabu, itakuwa kifungo gerezani kwasababu hukumu ya kifo haitumiki kwa mashtaka kama hayo.

Macho yote yalikuwa yameelekezwa kwa Soltani, anayeshikiliwa katika gereza la Karaj viungani mwa Tehran tangu kukamatwa kwake, na ambaye anakabiliwa na mashtaka ya propaganda dhidi ya mfumo wa Kiislamu wa Iran na kuendana kinyume na usalama wa taifa.

Hayo yanajiri saa chache kabla ya kufanyika kwa mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ulioitishwa na Marekani.