1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya wafu kutokana na mafuriko nchini Kongo yaongezeka

6 Mei 2023

Idadi ya waliopoteza maisha kutokana na mafuriko makubwa katika eneo la mashariki ya Kongo imeongezeka. Hadi kufikia sasa watu wapatao 182 wamekufa baada ya mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi kutokea.

https://p.dw.com/p/4QzBR
Kongo I Treffen zwischen EACRF und  M23-Rebellen
Picha: Guerchom Ndebo/AFP

Idadi ya waliopoteza maisha kutokana na mafuriko makubwa katika eneo la mashariki ya Kongo imeongezeka. Hadi kufikia sasa watu wapatao 182 wamekufa baada ya mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi kutokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Gavana wa eneo la Kivu Kusini Théo Ngwabidje, amethibitisha vifo vya watu hao kwa shirika la Habari la Ujerumani (dpa ). Amesema idadi zaidi ya watu waliokufa kwenye maafa hayo inatarajiwa kuendelea kuongezeka. Rais Félix Tshisekedi ametangaza siku ya Jumatatu kuwa ya maombolezo ya kitaifa. Msemaji wa serikali, Patrick Muyaya, ameeleza kuwa baadhi ya mawaziri watakwenda kwenye eneo la tukio kwa ajili ya kuratibu misaada na jinsi ya kusimamia shughuli za kuyakabili maafa hayo. Msimu wa mvua kubwa kwa kawaida kwenye mkoa wa Kivu Kusini unatarajiwa kudumu hadi mwisho wa mwezi huu wa Mei. Nchi jirani na Kongo pia katika siku za hivi karibuni zimekabiliwa na mafuriko makubwa, ambayo yamesababisha vifo vya watu 127 nchini Rwanda na watu sita nchini Uganda.