Idadi ya waliokufa Afrika Kusini kufuatia mafuriko yakaribia 60 | Masuala ya Jamii | DW | 13.04.2022
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Idadi ya waliokufa Afrika Kusini kufuatia mafuriko yakaribia 60

Idadi ya watu waliofariki kufuatia mafuriko na maporomoko ya udongo Afrika Kusini imeongezeka na kufikia watu 59. Hali hiyo imesababishwa na mvua kubwa katika mji wa Durban na maeneo ya jirani ya mkoa wa Kwazulu Natal.

Taarifa ya mamlaka ya mji wa Durban imesema mafuriko hayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa makaazi na miundombinu kutoka maeneo ya vijijini, vitongoji hadi maeneo ya kifahari. 

Mvua zilizonyesha kwa siku kadhaa zimesababisha maeneo kufurika, kubomoa nyumba na kuharibu miundombinu huku maporomoko ya ardhi yakilazimisha huduma za treni kusitishwa. 

Idara ya kudhibiti majanga katika jimbo la KwaZulu-Natal, imewataka watu kusalia majumbani mwao na kuamuru wale wanaoishi katika maeneo ya mabondeni kuhamia maeneo yenye muinuko. 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com