1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Hezbollah yafyetua maroketi zaidi ya 100 kuilenga Israel

Josephat Charo
12 Machi 2024

Kundi la Hezbollah nchini Lebanon limesema limevurumisha maroketi zaidi ya 100 hivi leo kuyalenga maeneo ya jeshi la Israel

https://p.dw.com/p/4dQF6
Mashambulizi ya kundi la Hezbollah yailenga Israel
Mashambulizi ya kundi la Hezbollah yailenga IsraelPicha: Jalaa Marey/AFP/Getty Images

Katika taarifa yake, kundi hilo limesema limefyetua maroketi aina ya katyusha leo asubuhi kuzilenga kambi mbili za jeshi kujibu mashambulizi ya Israel kwa watu wao, vijiji na miji, shambulizi la hivi karibuni likifanywa katika mji wa Baalbek ambapo raia mmoja aliuliwa.

Hapo jana shambulizi la jeshi la kutokea angani la Israel karibu na mji wa mashariki wa Baalbek lilimuua mtu mmoja, katika uvamizi wa pili dhidi ya ngome ya Hezbollah tangu makabiliano ya mpakani yalipoanza.