Hertha Berlin kileleni mwa Bundesliga | Michezo | DW | 09.03.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Hertha Berlin kileleni mwa Bundesliga

Andrey Veronin atia mabao 3 pekee dhidi ya Cottbus.

default

Herta Berlin yatamba:

Simba wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo wanaguruma huko Abidjan na watoroka na Kombe la Afrika hadi Kinshasa baada ya kuilaza jana Ghana mabao 2:0. Tutaenda Kinshasa kusikia shangwe na shamra shamra.

Patashika katika shirikisho la dimba la Tanzania baada ya Taifa kuaga na mapema kombe la Afrika huko Ivory Coast.

Finali ya Kombe la Afrika kwa wachezaji wanaocheza nyumbani afrika ,imemalizika huko Abidjan jana kwa ushindi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo .Kongo ilizaba Ghana mabao 2:0 na kutoroka na kombe hilo hadi Kinshasa. Kufuatia ushindi huo ,serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imetangaza siku ya leo ni siku kuu kwa wakongomani.

Katika Bundesliga,Bayer Leverkusen ilishindwa jana kutumia nafasi ya kuilaza Bochum iliocheza na wachezaji 10 ili kuparamia kileleni mwa bundesliga.Leverkusen ilimudu sare bao 1:1 na Bochum wakati Frankfurt iliondoka pia suluhu na Armenia Bielefeld.

Changamoto iliokodolewa macho zaidi ilikua jumamosi pale mabingwa Bayern munich walipotertemka uwanjani nyumbani kuicheza na Hannover. Mpambano huu ulitanguliwa na pigo la kati ya wiki iliopita katika kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani (DFB) ilipotimuliwa nje ya kombe hilo na Leverkusen kwa mabao 4-2.

Ikelewa kuwa mpambano huo wa jumamosi ni wa kufa -kupona na hatima yake inategemea ushindi, kocha Jurgen klinsmann, aliwapa akina Miroslav klose na Lukas Podolski jukumu moja tu-ushindi na wao hawakumvunja moyo kama munira Mohammed anavyosimulia:

Bayern Munich iliizaba Hannover mabao 5-1.Lakini ilikua Hannover iliotangulia kutia bao pale mshambulizi wao Steiner alipouchapa mkwaju mkali ulionasa katika lango la Munich. Klinsmann akihisi mambo yameanza tena kwenda kombo, mkondo wa mchezo uligeuka ghafula -baada ya klose kutia mabao 2 na Podolski bao 1 .Mwishoe, Munich iliondoka na ushindi wazi.

Akielezea kuridhika na ushindi huo,Philip Lam,beki mashuhuri wa Bayern munich alisema:

"Leo tulibidi kwa kila hali kushinda.Iwapo haya ni mabadiliko mema kwetu,sijui,lakini natumai wiki ijayo tutaendelea kusonga mbele zaidi ili kupata n afasi ya kuibuka tena mabingwa wa Ujerumani."

Nae mshambulizi hatari wa Munich alietia mabao 2,Miroslav Klose amesema:

"Ilikua muhimu tumeteketeleza tulionuia na kwamba kila mmoja alijua tumefikia ukingoni kutumbukia na hivyo natumai leo tumejiokomboa."

Munich lakini, bado haiko kileleni, bali ni Hertha Berlin inayoongoza kwa pointi zake 46 .Hertha iliikomea Cottbus mabao 3:1 -yote yakitiwa na Muukrain Andry Veronin.Hoffenheim ilimudu suluhu tu 0:0 na Werder Bremen.Wolfsbur walijipatia ushindi wao wa 5 mfululizo kwa kuizaba Karlsruhe bao 1-0 wakati hamburg ilikomewa mabao 4-1 na Borussia Moenchengladbach inayoburura mkia. FC Cologne,ilikomewa bao 1:0 na Schlake hapo ijumaa ikipata pigo lake la kwanza tangu kuingia mwaka mpya.

Ama huko Uingereza,Manchester United itakumbana na Everton katika nusu-finali ya Kombe la FA -hii inatokana na kura iliopigwa jana .Mpambano huo utakua marudio ya finali ya kombe hilo za mwaka 1995 na 1985.Nusu-finali nyengine itakua kati ya helsea ama na Arsenal au Hull City zinazocheza robo-finali yao baadae.

Katika Ligi ya Itali-Serie A, AC Milan imefaulu kurefusha mkataba wa stadi wa uingereza David Beckham alieazimwa kutoka klabu ya Los Angeles Galaxy.Beckham,ataweza sasa kusalia na AC milan hadi mwisho wa msimu huu.

Akiwa na umri wa miaka 33, Beckham alijiunga na AC Milan desemba mwaka jana kwa kuazimwa tu hadi Machi 9 hii leo.Kwa muujibu wa mapatano ,Beckkham ataichezea AC Milan hadi juni 30 na halafu atajiunga tena na Los Angeles galaxy hapo Julai mosi kuanza kwa msimu mpya unaomalizika mwishoni mwa Novemba.Nahodha huyo wa zamani wa Uingerteza atakuwa huru tena kusalia na kalbu hiyo ya california kwa miaka 2 zaidi au hata kujiunga na klabu nyengine.

Katika La Liga-ligi ya spain,ushindi wa jana wa mabao 2-1 dhidi ya Ameira , umejongeza jana Sevilla karibu nafasi ya tatu ya ngazi ya Ligi.Alikuwa frederic kanoute wa Mali alietia bao la kwanza la Sevilla dakika 5 tu baada ya dimba kuanza.Renato akahetimisha kwa bao la 2 kabla Alvaro Negredo kutia bao la kufuta machozi la Almeira.Mabingwa Real Madrid walimudu sare bao 1:1 na Ateltico Madrid.Real sasa iko pointi 6 nyuma ya viongozi wa Ligi FC Barcelona ilioizaba Athletico Bilbao mabao 2:0.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com