HEILEGENDAMM: Polisi wapambana na waandamanaji. | Habari za Ulimwengu | DW | 07.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HEILEGENDAMM: Polisi wapambana na waandamanaji.

Polisi wa Ujerumani wametumia mabomba ya maji kuwatawanya mamia ya waandanamaji kutoka barabara zinazoelekea kwenye eneo la mkutano wa wakuu wa mataifa manane yaliyostawi kiviwanda.

Waandanamaji wanaopinga utandawazi walifunga barabara moja kuu na kwa mujibu wa makundi ya wanaharakati waandanamaji wengine walifunga barabara nyingine inayoelekea katika mji wa kitalii wa Heilegendamm.

Kiasi askari-polisi wanane walijeruhiwa baada ya kuvurumishiwa mawe na waandamanaji waliokabiliana na polisi walipotaka kuukaribia ukuta wa usalama kwenye hoteli ya kifahari ambako viongozi hao wanakutana.

Watu themanini na wanane wameshikiliwa na polisi kutokana na tukio hilo.

Kundi moja linalopinga utandawazi limesema watu elfu kumi walishiriki kwenye maandamano hayo ambayo lilisema yalikuwa ya amani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com