1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Hassan Rouhani

Hassan Rouhani ni mwansiasa wa Iran na rais wa 7 wa Jamhuri hiyo ya Kiislamu tangu Agosti 3, 2013. Pia aliwahi kuwa mwansheria, mwanadiplomasia wa zamani na kiongozi wa kidini.

Amekuwa mjumbe wa baraza la wataalamu la Iran tangu 1999, mjumbe wa baraza la manufaa tangu 1991, na mjumbe wa baraza la juu la usalama wa taifa tangu 1989. rouhani alikuwa naibu spika wa bunge la nne na la tano, na katibu wa baraza la taifa la usalama wa taifa kuanzia 1989 hadi 2005. Katika wadhifa wa baadae, alikuwa mpatanishi mkuu pamoja na mataifa matatu ya Umoja wa Ulaya - Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kuhusu teknolojia ya nyuklia ya Iran. Ukurasa huu ni mkusanyiko wa maudhui za DW kuhusu Rouhani.

Onesha makala zaidi