1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Iran autetea mkataba wa nyuklia

Lilian Mtono
9 Juni 2021

Rais wa Iran Hassan Rouhani amejitetea baada ya kushambuliwa vikali kwenye mjadala uliowakutanisha wagombea wa urais akisema wakosoaji wake wana tamaa ya madaraka yanayowasababishia kupoteza kumbukumbu.

https://p.dw.com/p/3udFz
Iran Präsident Hassan Rohani
Picha: Iranian Presidency/ZUMAPRESS/picture alliance

Katika mjadala huo wa pili wa wagombea urais, wagombea wenye msimamo mkali kwa mara nyingine waliyabeza matumaini ya utawala wa Rouhani kuhusu mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 na mataifa yenye nguvu duniani ambao unasuasua.

Rouhani aliyeonekana mwenye hasira alitoa matamshi hayo yaliyowalenga wakosoaji wake, kupitia hotuba yake kwa baraza la mawaziri iliyorushwa kwenye televisheni. 

soma zaidi: IAEA yataka majibu kutoka Iran kuhusu shughuli za nyuklia

Amesema wanasiasa wenye misimamo mikali, ambao kwa muda mrefu wanayakosoa makubaliano hayo wanatakiwa kuchunguzwa kuhusiana na iwapo wanataka nafuu ya vikwazo kwa kurejea kwenye makubaliano hayo yaliyozorota baada ya Donald Trump kujiondoa mwaka 2018.