HARARE: Tsvangirai atoa wito kumtenga Mugabe | Habari za Ulimwengu | DW | 29.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HARARE: Tsvangirai atoa wito kumtenga Mugabe

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai ametoa wito kwa nchi za kusini mwa Afrika kumtenga Rais Robert Mugabe anaetawala kwa mabavu.Katika mahojiano yake na gazeti la Kijerumani,”Frankfurter Rundschau”,Tsvangirai amesema majadiliano yapaswa kufanywa hivi sasa. Vile vile amemtuhumu Rais Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini kuwa anamuunga mkono Mugabe.Siku ya Jumatano,Tsvangirai na wanasiasa wengine wa chama chake cha upinzani MDC walikamatwa na polisi lakini baadae wakaachiliwa huru.Kama majuma mawili yaliyopita,Tsvangirai alikamatwa na polisi na akapigwa vibaya sana alipokuwa kizuizini.Tukio hilo lilizusha lawama kali sehemu mbali mbali duniani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com