1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas yatengeza njia mpya kwa wapalestina wakimbie Gaza

25 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CxlM

Wapalestina leo mchana wamekuwa na hekaheka ya kurejea katika makaazi yao katika Ukanda wa Gaza wakati Misri ilipokuwa ikijaribu kuufunga mpaka kati yake na eneo hilo.

Maafisa wa usalama wa Misri ambao wamekuwa tangu asubuhi wakijaribu kuufunga mpaka huo wamefyatua risasi angani kujaribu kuwazuia watu wasivuke mpaka na kuingia Misri.

Wanamgambo wa Hamas leo wametumia tingatinga kukata waya wa sing´esing´e karibu na kivuko cha mpakani cha Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza kujaribu kutengeneza njia mpya kuwawezesha mamia ya wapalestina wakimbie Gaza kwenda Misri.