Habusi mmoja aliyekua akishikiliwa na FARC nchini Colombo amefanikiwa kutoroka | Habari za Ulimwengu | DW | 06.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Habusi mmoja aliyekua akishikiliwa na FARC nchini Colombo amefanikiwa kutoroka

Bogota:

Waziri wa zamani wa misaada ya maendeleo nchini Colombia aliyetekwa nyara tangu miaka sita iliyopita na wanamgambo wa FARC,Fernando Araujo,amefanikiwa kutoroka .Araujo ametoroka kufuatia mapigano kati ya waasi na vikosi vya jeshi la serikali kaskazini mwa nchi hiyo ya Latin America.Mwanasiasa huyo aliyekondeana amesema alijificha siku tano msituni hadi wanajeshi wa serikali walipomgundua.Araujo alikua miongoni mwa mahabusi 58 wanaoshikiliwa na wamgambo wa FARC .Alitekwa nyara december mwaka 2000 katika mji wa mwambao wa Cartagena.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com