Eneo la Sahel barani Afrika ndio kitovu cha ugaidi duniani
20 Machi 2026
Faharasa hiyo iliyoandaliwa na taasisi ya Taasisi ya Uchumi na Maswala ya Amani imeziorodhesha nchi 163 kwa muda wa miaka 13 kulingana na athari za "ugaidi" kwa kuzingatia viashiria kama vile idadi ya mashambulizi, vifo, majeruhi na mateka.
Ripoti hiyo inafafanua ugaidi kama "tishio la kimfumo au matumizi ya nguvu, yanayofanywa na watendajizopo madarakani."
Mnamo 2024, zaidi ya nusu ya vifo 7,555 vilivyotokana na "ugaidi" duniani kote viliorodheshwa kutokea katika eneo la Sahel, kwenye ukanda wenye ukame unaoenea kandoni mwa ukingo wa Afrika kusini mwa jangwa la Sahara kutokea Bahari ya Atlantiki hadi kwenye Bahari Nyekundu.
Upi mwelekeo
Taasisi ya Uchumi na Maswala ya Amani yenye makao yake makuu nchini Australia imesema mwelekeo huo haukubadilika sana mwaka wa 2025. Ripoti hiyo imesema. "Kitovu cha ugaidi kimehama kutoka Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, hadi eneo la Sahel la Kusini mwa Jangwa la Sahara."
Hata hivyo, Nina Wilén ambaye ni mkuu wa Mpango wa Afrika katika Taasisi ya Egmont ya Mahusiano ya Kimataifa na mwandishi wa kitabu kuhusu kulilinda eneo la Sahel, kinachoitwa ‘Securitizing the Sahel' amesema ndio maana sio jambo la kushangaza kwa ripoti hiyo kuyahusisha mashambulizi mengi katika eneo la Sahel na makundi ya Jama'at Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM ) na lile linalojiita Dola la Kiislamu (IS).
Burkina Faso ni nchi iliyoathiriwa zaidi duniani kwa miaka miwili mfululizo. Niger, imo katika nafasi ya tatu ikiwa na ongezeko la matukio ya "ugaidi" katika mwaka wa 2025.
Nigeria imepanda hadi nafasi ya nne kwenye orodha, huku watu 750 wakiuawa mwaka wa 2025, mauyji hayo yameongezeka kwa asilimia 46 kutoka mwaka uliotangulia.
Makundi hayo ya wapiganaji wenye misimamo mikali yanaendelea kukuza harakati zake hadi kwenye pwani za nchi za Afrika Magharibi, hasa Benin, ambayo imepanda hadi nafasi ya 19 kutoka nafasi ya 26 kwenye orodha ya "ugaidi" duniani kote.