1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na Haki

Duterte kukabiliwa na kesi ya ICC mnamo Februari 23

26 Januari 2026

Rais wa zamani wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, atakabiliwa na kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) mwezi ujao.

https://p.dw.com/p/57UQ2
Ufilipino Manila 2024 | Rais wa zamani Rodrigo Duterte mbele ya kamati ya Seneti kuhusu vita vya kupambana na dawa za kulevya
Rais wa zamani wa Ufilipino, Rodrigo DutertePicha: Aaron Favila/AP Photo/picture alliance

Rais wa zamani wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, atakabiliwa na kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) mwezi ujao. Uamuzi huo umetolewa na majaji wa ICC mapema leo Jumatatu, baada ya kuzikataa hoja kwamba kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80 hawezi kushiriki kutokana na hali ya afya yake.

Duterte atafikishwa katika hatua ya uthibitisho wa mashitaka kuanzia Februari 23, ambapo majaji wataamua kama madai ya upande wa mashtaka yana nguvu ya kutosha kuendelea hadi kesi ikamilike.

Waendesha mashtaka wa ICC wamemfungulia Duterte mashitaka matatu ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, wakimtuhumu kuhusika katika mauaji takribani 76 kama sehemu ya kampeni yake ya kupambana na walanguzi wa dawa za kulevya.

Duterte alikamatwa Manila mnamo Machi 11, na tangu wakati huo amekuwa akishikiliwa katika kitengo cha mahabusu cha ICC nchini Uholanzi.