1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Duru ya kwanza ya mazungumzo ya Hamas yamalizika vyema

7 Oktoba 2025

Duru ya kwanza ya mazungumzo kuhusu Gaza kati ya Hamas na wapatanishi imekamilika "katika mazingira chanya", nchini Misri. Hayo ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vinavyohusishwa na serikali ya Misri.

https://p.dw.com/p/51Zn3
Misri Cairo 2014 | Mahmoud Abbas akutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu
Rais wa Palestina Mahmoud AbbasPicha: Amr Nabil/AP Photo/picture alliance

Al-Qahera News, chombo kinachohusishwa na ujasusi wa serikali, kiliripoti kuwa mazungumzo yataendelea, pia kati ya Hamas na wapatanishi katika mji wa mapumziko wa Sharm El-Sheikh, ambako ujumbe wa Israel uliwasili jana Jumatatu.Israel na Hamas wanatarajiwa kushiriki mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kuhusu pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu kubadilishana mateka na wafungwa pamoja na kusitisha mapigano kwa muda mrefu.