1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Cohen: Hatua za Israel ni sawa na 'utawala wa moja kwa moja'

10 Februari 2026

Waziri wa Nishati wa Israel Eli Cohen amesema Jumanne kwamba hatua zilizochukuliwa na serikali za kuimarisha udhibiti wa Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa ni sawa na kujitangazia "mamlaka ya moja kwa moja".

https://p.dw.com/p/58T2K
Waziri wa nishati wa Israel  Eli Cohen akiwa Larnaca
Waziri wa Nishati wa Israel Eli Cohen amesema hatua mpya za Israel kuelekea Ukingo wa Magharibi zinafanana na utawala wa moja kwa moja kwenye eneo hiloPicha: Petros Karadjias/AP Photo/picture alliance

Cohen ameiambia Radio ya Jeshi la Israel, hatua hizo zinathibitisha kwa dhati kwamba hakutakuwa na taifa la Palestina.

Maoni ya Cohen yanafuatia matamshi kama hayo yaliyotolewa na wajumbe wengine wa serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, akiwemo Waziri wa Fedha Bezalel Smotrich na Waziri wa Ulinzi Israel Katz, ambayo pia yanaondoa kabisa hata mamlaka kidogo aliyonayo Mamlaka ya Palestina na haijulikani ni kwa kiwango gani inaweza kuwapinga.

Wapalestina, nchi za Kiarabu na makundi ya haki za binadamu wameita hatua hizo zilizotangazwa Jumapili kuwa ni unyakuzi wa eneo hilo, linalokaliwa na Wapalestina wapatao milioni 3.4, wanaopigania taifa lao huko siku za usoni.