1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yapigia debe kuboreshwa mahusiano na Korea Kusini

Saleh Mwanamilongo
13 Mei 2024

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema nchi yake na Korea Kusini zinakabiliwa na matatizo yanayoongezeka, lakini amesema zinapaswa kuimarisha ushirikiano wao bila kuingiliwa kati.

https://p.dw.com/p/4fo3V
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa China, Wang Yi.
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa China, Wang Yi.Picha: Willy Kurniawan/AFP

Wang Yi ameyasema hayo kufuatia mazungumzo na mwenzie wa Korea Kusini Cho Tae-Yul, mjini Beijing.

Kwa upande wake Cho Tae-yul, amesema nchi hizo mbili zinahitajika kuendeleza ushirikiano wao, na kuhakikisha kuwa tofauti zao zisigeuke kuwa mzozo.

Waziri huyo wa Korea Kusini, aliwaambia wafanya biashara wa nchi yake, kwamba uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi yake na China unakabiliwa na changamoto, kutokana na ushindani mkali unaozidi kuongezeka hasa katika sekta ya teknolojia.

Cho aliwasili Beijing mapema leo Jumatatu, ikiwa ni safari yake ya kwanza nchini China tangu aingie madarakani mwezi Januari. Hiyo pia ni ziara ya kwanza kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini nchini China kwa zaidi ya miaka sita.