CAIRO:Al Qaida wadai kuhusika na shambulizi | Habari za Ulimwengu | DW | 26.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CAIRO:Al Qaida wadai kuhusika na shambulizi

Muungano wa kisunni unaongozwa na tawi la Al Qaida nchini Iraq, umedai kuhusika na shambulizi la kujitoa mhanga la hapo jana dhidi ya mkutano uliyoitishwa na Marekani kati ya viongozi wa kisunni na kishia kwenye jimbo la Baquoba ambapo watu 15 waliuawa.

Katika taarifa waliyoituma kwenye mtandao kundi hilo limedai kutimiza ahadi yake ya kuliadhibu kile wanachoita taifa lililoasi dini.

Ujumbe huo umesema kuwa mmoja wa simba wa kundi hilo, Abu Omar al Kurdi Brigades alifanikiwa kujilipua kwenye mkutano huo ndani ya msikiti, ambapo miongoni mwa waliyokufa ni mkuu wa polisi wa jimbo la Baquoba.

Zaidi ya watu 30 walijeruhiwa akiwemo gavana wa jimbo na askari wawili wa Marekani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com