1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAF yasogeza mbele michuano ya Kombe la Afrika la Wanawake

5 Machi 2026

Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) limethibitisha kuahirishwa kwa Kombe la Mataifa ya Afrika la Wanawake (WAFCON) hadi Julai-Agosti. Michuano hiyo awali ilipangwa kuchezwa Machi hadi Aprili.

https://p.dw.com/p/59s9H
Timu ya wanawake ya kandanda ya Nigeria ya Super Falcons ya Nigeria
Nigeria ndio mabingwa watetezi baada ya kunyakua kombe katika mashindano ya 2024Picha: Adekunle Ajayi/NurPhoto/IMAGO

Mashindano haya yanatumika kama maandalizi ya Kombe la Dunia la Wanawake la 2027, ambapo timu nne za Afrika zitafuzu moja kwa moja, na mbili zaidi zitashiriki katika mechi za kufuzu za kimataifa.

Awali, WAFCON ilipangwa kuchezwa kuanzia Machi 17 hadi Aprili 3, lakini wenyeji Morocco walishinikiza mabadiliko ya tarehe kutokana na kile ambacho CAF inakielezea kama "hali zisizotarajiwa".

"Baada ya mazungumzo kati ya CAF na washirika wake, FIFA na wadau wengine, CAF iliamua kupanga upya tarehe za TotalEnergies CAF WAFCON 2026, hadi 25 Julai - 16 Agosti 2026 ili kuhakikisha mafanikio ya tamasha hili muhimu la wanawake, kutokana na hali fulani zisizotarajiwa," ⁠CAF ilisema katika taarifa siku ya Alhamisi, bila kutoa maelezo zaidi kuhusu sababu ya kuahirishwa.

"Maandalizi ya TotalEnergies CAF WAFCON 2026 yanaendelea na pande zote zina uhakika kwamba yatafanikiwa sana."

Idadi ya timu zinazoshindana katika michuano hiyo imeongezwa hadi 16 kwa mara ya kwanza, ambapo Nigeria ndio mabingwa watetezi baada ya kunyakua kombe katika mashindano ya 2024, yaliyofanyika mwaka jana baada ya kuahirishwa pia.

Reuters