Bobi Wine asema anapewa hifadhi na raia wa Uganda
22 Januari 2026
Matangazo
Akizungumza na shirika la habari la Ufaransa AFP, Wine aliyekamatwa na kuteswa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2021 ila akashiriki uchaguzi wa wiki iliyopita, amesema kuwa kwa sasa yuko mafichoni na anapewa hifadhi na raia wa kawaida tu huko Uganda, wakati ambapo familia yake imezuiwa kutoka nje kwa kipindi cha wiki moja sasa.
Rais Yoweri Museveni na mwanawe Muhoozi Kainerugaba ambaye ndiye mkuu wa majeshi, wamewataja viongozi wa upinzani kama "magaidi."
Muhoozi mwenye umri wa miaka 51 na ambaye ameweka wazi nia yake ya kumrithi babake, ametishia kumtafuta Wine na kumuua.
Museveni katika uchaguzi wa Januari 15, alichaguliwa kwa muhula wake wa saba katika matokeo ya uchaguzi yaliyopingwa na upinzani.