1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken amuhimiza Netanyahu kuruhusu misaada Gaza

7 Februari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken leo ametoa wito wa hatua zaidi kuchukuliwa ili kuingiza misaada zaidi Gaza.

https://p.dw.com/p/4c8n1
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken (kushoto) akikaribishwa na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, mjini Tel Aviv.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken (kushoto) akikaribishwa na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, mjini Tel Aviv.Picha: Amos Ben-Gershom/dpa/picture alliance

Akizungumza baada ya mkutano na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, Blinken alisema hatua zaidi zinazostahili kuchukuliwa mbali na kuwasilishwa kwa misaada, ndilo lengo hasa la ziara na mikutano yake.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani ameonesha matumaini kuhusiana na suala la makubaliano ya kuwaachia mateka walio mikononi mwa wanamgambo wa Hamas, ila akasema kuwa juhudi zaidi zinahitajika.

Haya yanafanyika wakati ambapo jeshi la Israel likisema kuwa limegundua na kuliharibu handaki linalotumiwa na viongozi wa kundi la Hamas kuwashikilia mateka katika mji muhimu wa Gaza wa Khan Younis.

Jeshi hilo linasema handaki hilo lina urefu wa zaidi ya kilomita moja.