1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken afanya mazungumzo ya faragha na mwenzake wa Uturuki

Saumu Mwasimba
6 Novemba 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani amefanya mazungumzo ya faragha na mwenzake wa Uturuki mjini Ankara.

https://p.dw.com/p/4YSHI
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na mwenzake wa Uturuki Hakan Fidan
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na mwenzake wa Uturuki Hakan FidanPicha: Jonathan Ernst/AP Photo/picture alliance

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amefanya mazungumzo ya faragha  leo Jumatatu na mwenzake wa Uturuki  Hakan Fidan mjini Ankara kujaribu kutuliza hasira za nchi hiyoambayo ni mmoja wa washirika wake muhimu wa kimkakati. 

Ziara ya Blinken Uturuki ni ya kwanza nchini humo tangu Israel ilipoingia vitani na kundi la Hamas kujibu mashambulizi yaliyofanywa Oktoba 7 na kundi hilo katika ardhi ya Israel. 

Polisi walitumia gesi ya kutowa machozi na mabomba ya maji dhidi ya umma wa mamia ya watu walioandamana katika kambi ya jeshi la wanaanga la Marekani Kusini Mashariki mwa Uturuki, saa chache kabla ya Blinken kuwasili jana Jumapili.

Soma pia:Blinken afanya ziara ya kushtukiza Ukingo wa Magharibi

Rais Recep Tayyip Erdogan amekwenda kulitembelea eneo la  Kaskazini Mashariki mwa nchi yake hii leo katika hatua inayoonekana ni ya kumpuuza mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Marekani.

Vita vya Gaza vinatishia kuhatarisha mahusiano ya Marekani na Uturuki ambaye ni mwanachama wa Nato na ambayo ina ushawishi mkubwa katika migogoro ya eneo zima la Mashariki ya Kati.