BERLIN : Gaidi Monhaupt aachiliwa kwa dhamana | Habari za Ulimwengu | DW | 12.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Gaidi Monhaupt aachiliwa kwa dhamana

Mahkama ya Ujerumani imepitisha hukumu ya kumuachilia kwa dhamana kutoka gerezani Brigitte Mohnhaupt mwanachama wa zamani wa kundi lililovuma kwa ubaya la Baader-Meinhof.

Mohnhaupt ametumikia kifungo cha miaka 24 gerezani kwa kuhusika kwake katika vitendo vya utekaji nyara na mauaji katika miaka ya 1970 na kundi hilo la Baader-Meinhof ambalo pia lilikuwa likijulikana kwa jina jengine la Red Army.Kiongozi huyo wa ugaidi amepatikana na hatia ya mauaji ya watu tisa ambapo wahanga ni pamoja na mtaalamu wa benki na rais wa shirikisho la waajiri.

Mwanamama huyo aliomba kuachiliwa na mapema kutoka gerezani baada ya kutumikia kipindi cha muda mfupi kwa mujibu wa sheria ya Ujerumani. Mfungwa mwengine mashuhuri wa kundi hilo Christian Klar naye pia anapigania kuachiliwa na mapema kutoka gerezani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com