BEIJING: Daraja laporomoka na kuuwa watu 36
17 Agosti 2007Matangazo
Idadi ya watu waliopoteza maisha yao baada ya daraja kuporomoka,kusini mwa China,imefikia 36 na wengine 23 bado hawajulikani walipo.Daraja hilo katika wilaya ya Hunan,lilikuwa bado likijengwa. Maafisa wanasema,kuna matumaini madogo ya kukuta watu walionusurika,kwa sababu wakuu wa afya wameanza kunyunyuiza dawa katika maji,ili kuzuia uambukizaji wa magonjwa.