Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuamua "hadhi" ya Palestina
10 Mei 2024Mnamo Aprili 18, Marekani ilipinga azimio lililopata uungwaji mkono mkubwa, ambalo lingetoa mwanya kwa Palestina kutambuliwa kama mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa, lengo ambalo Wapalestina wamelipigania kwa muda mrefulakini Israel imekuwa ikipambana kulizuia.
Soma pia: Je, Palestina inayotambulika itasaidia kumaliza mzozo wa Gaza?
Naibu balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Robert Wood alisema kwamba Washington inapinga azimio hilo la Baraza Kuu, akiongeza kuwa njia pekee ya kupata uanachama kamili wa Palestina katika Umoja wa Mataifa ni kupitia mazungumzo na Israel.
Uhispania, Ireland na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Ulaya, zinapanga kulitambua taifa la Palestina Mei 21, kulingana na mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell.