1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Negroponte amekutana na al-Maliki

12 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsU

Naibu waziri wa nje wa Marekani John Negroponte amewasili mji mkuu wa Iraq,Baghdad kwa ziara ambayo haikutangazwa hapo kabla.Negroponte,ambae hapo awali alikuwa balozi wa Marekani nchini Iraq,amekutana na Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al-Maliki siku moja baada ya waziri mkuu mteule wa Uingereza,Gordon Brown,kuitembelea nchi hiyo iliokumbwa na machafuko.Brown ambae ni waziri wa fedha wa Uingereza,anatazamiwa kuchukua nafasi ya Tony Blair mwishoni mwa mwezi huu.