BAGHDAD : Mripuko wauwa 15 na kujeruhi 25 | Habari za Ulimwengu | DW | 25.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : Mripuko wauwa 15 na kujeruhi 25

Shambulio la kujitolea muhanga maisha kwa kutumia gari la mafuta kwenye kituo cha ukaguzi wa polisi katika kiunga cha mji wa Ramadi ulioko katikati ya Baghdad limeuwa watu 15 na kujeruhi wengine 25.

Polisi imesema gari hilo la mafuta limeripuka katika eneo lenye maduka kadhaa.Mripuko huo unakuja siku moja baada wanajeshi tisa wa Marekani kuuwawa na 20 kujeruhiwa katika shambulio la kujitolea muhanga maisha kwenye gari kaskazini mashariki mwa Baghdad.

Kundi lenye mafungamano na Al Qaeda nchini Iraq limedai kuhusika na shambulio hilo katika jimbo la Diyala ambalo ni baya kabisa dhidi ya majeshi ya nchi kavu ya Marekani kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miezi 16.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com