ATHENS:Moto wapungua nguvu na kasi | Habari za Ulimwengu | DW | 29.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ATHENS:Moto wapungua nguvu na kasi

Moto unaripotiwa kupungua kasi na nguvu nchini Ugiriki baaada ya kutatiza nchi hiyo kwa siku sita sasa.Kulingana na msemaji wa idara ya kuzima moto moto katika eneo la Peloponnese na kisiwa cha Evia bado haujazimwa ila umepungua nguvu.

Eneo hilo la rasi ya Pelopennese limeathirika zaidi kuliko yote na moto kusababisha vifo vya yapata watu 63.Helikopta 3 za kuzima moto vilevile nyingine mbili za kawaida zinaendelea kunyunyiza maji katika eneo la Eleia magharibi mwa Peloponnese ambako kumeripotiwa kutokea vifo vingi zaidi tangu siku ya Ijumaa.

Ndege 4 na helikopta moja zinaendelea kuzuima moto katika kisiwa cha Evia kilicho kaskazini mwa mji wa Athens.Moto ulisambaa katika maeneo mengi ila juhudi za kuzima moto zilifanikishwa na mvua kidogo iliyonyesha na kupunguza kasi ya upepo.

Zaidi ya wanajeshi alfu 2 na yapata wazima moto 800 wanashirikiana na ndege za helikopta kutoka mataifa zaidi ya kumi ili kupambana na moto huo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com