1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Athari za mgao wa umeme Tanzania

24 Novemba 2022

Kumekuwa na wasiwasi mkubwa nchini Tanzania kutokana na mgao wa umeme ambao umeathiri maeneo mengi.

https://p.dw.com/p/4K0pz
Irak Stromnetz Stromversorgung Stromleitung
Picha: Photoshot/picture alliance

Mamlaka nchini humo zinasema mgawo huo umesababishwa na hali ya ukame lakini wakosoaji wa mambo wanainyoshea kidole serikali kwa kushindwa kuweka vipaumbele vyake ili kuondokana na adha hiyo inayojitokeza mara kwa mara.

Kiasi cha umeme kinachoelezwa kupungua kinatajwa kufikia megawati 300 hadi 350 kwa siku.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la umeme Tanzania TANESCO Maharage Chande amesema kiwango cha maji katika maeneo kama Kihansi, Bwawa la Mungu na maeneo mengine kipo chini mno.

Kwa maana hiyo hali ya mgawo huo huenda ukaandeelea kuathiri wengi hadi mwishoni mwa mwezi ujao wa Disemba ingawa shirika hilo linasema limeweka mipango kadhaa kurejesha uzalishaji wa umeme.